Pichani kabla ya Safari,Amigolas akiwa na wasanii wenzake wakati wa kuelekea jijini London.
Wasanii waliopotea: Miraji Shakashia ‘Shaka Zuru’ (wa kwanza kulia waliochuchumaa) na Amigoras (wa tatu kushoto waliosimama) wakiwa na wasanii wenzao pamoja na viongozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Na Musa Mateja WANAMUZIKI wawili wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Hamis Amigolas na Miraji Shakashia ‘Shaka Zuru’, wamepotea nchini Uingereza na kusababisha kuachwa na ndege huku bosi wao, Asha Baraka akihaha kujua kilichojiri.
Chanzo chetu cha habari kimesema kuwa Novemba 6, mwaka huu, wanamuziki wa bendi hiyo walirejea Bongo lakini wawili hao hawakuwepo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, wawili hao walikwenda kununua zawadi za kurudi nazo Bongo lakini wakasahau geti la kuingilia uwanja wa ndege, jijini London, Uingereza.
“Kusema kweli Amigolas na Shaka Zuru walikwenda kununua zawadi ili warudi nazo nyumbani, lakini walishindwa kufahamu geti sahihi la kuingilia uwanja wa ndege wakati wakirudi, maana kutoka getini hadi kufika uwanjani kuna umbali mrefu,” kilisema chanzo.
Wanamuziki wengine wa bendi hiyo walirejea nchini na kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere na baadhi ya mashabiki wao.
WANAMUZIKI wawili wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Hamis Amigolas na Miraji Shakashia ‘Shaka Zuru’, wamepotea nchini Uingereza na kusababisha kuachwa na ndege huku bosi wao, Asha Baraka akihaha kujua kilichojiri.
0 Comments