Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Somalia inahamia Mogadishu kutoka Nairobi, Katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon ametangaza hayo akiwa katika ziara nadra kutokea nchini humo.
Katibu huyo mkuu wa UN ni kiongozi wa ngazi za juu kuzuru mji huo ulioharibiwa na vita kwa miaka mingi.(Pichani akisalimiana na baadhi ya viongozi na wananchi nchi Somalia).Bwana Ban Ki Moon pichani katikati mwenye miwani
Alikuwa amevaa fulana isiyopenyeza risasi alipokaribishwa uwanja wa ndege na waziri mkuu wa Somalia.
Wapiganaji wa kiislam wanapigana na vikosi vya serikali inayoungwa mkono Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Somalia imekuwa katika vita kwa miongo miwili na haina serikali yenye nguvu tangu mwaka 1991.
Ziara ya Bw Ban inakuja siku moja baada ya mapigano makali kutokea mjini Mogadishu katika kipindi cha miezi kadhaa.
Barabara zote kubwa zilifungwa na ndege kuingia na kutoka Mogadishu zilifutwa kwa sababu za kiusalama.
Bw Ban alikuwa anatarahiwa kujadili hali ya kisiasa Somalia na pia njaa ambayo imetangazwa kuwa janga baada ya maeneo ya kusini kukumbwa na ukame mkali.
0 Comments