Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Handeni
. Mahakama ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewahukumu Raia 103 wa Somalia, kwenda Jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Handeni Jonathan Mgongolwa, mwendesha mashitaka wa Idara ya uhamiaji wilayani humo ASP Charles Kasambula, alidai kuwa wasomali hao walikamatwa na Polisi katika maeneo mawili tofati wilayani humo wakiwa njiani kuelekea nchini Malawi bila ya kufuta taratibu za kiuhamiaji.
Watuhumiwa wote walikiri shitaka hilo na Hakimu Mgongolwa akaamru kuwahukumu kwenda Jela mwaka mmoja na kwamba mara wamalizapo kifungo chao, wasomali hao wasafirishwe kurudishwa makwao katika nchi waliotoka.
Wakati wa hukumu hiyo, Hakim Mgongolwa amesema amelazimika kutoa adhab hiyo ili iwe fundisho kwa wageni wengine wanaotaka kuingia hapa nchini kufuata taratibu na sheria zikiwemo zile za kimataifa zinazomlazimu kila mgeni kuheshimimu mipaka na taratib za nchi anayopanga kuingie ama kupitia akiwa njiani kuelekea katika taifa lingine.
Wasomali hao hao ambao wote ni wanaume wenye umri kati ya miaka 20 na 30, walikamatwa na Polisi wilayani Handeni mwishoni mwa wiki iliopita wakati wa operesheni maalum ijulikanayo kama funga mwaka bila uhalifu inayoendeshwa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Katika hata nyingine Jeshi la Polisi mkaoni Tanga limesema linafuatilia nyendo za mawakala wanaopokea wahamiaji haram na kwasafirishwa kwa magendo kwenda katika mataifa mengine.
Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Costantino Masawe, amesema kuwa pamoja na mawakala hao, pia Polisi inayafuatilia magri ya mizigo na madereva wanaotumika kuwasafirisha wasomali hao ili wakamata na kuwafikisha mahakamani.
Kamanda Masawe amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu vikiwemo vile vya usafirishaji haramu wa binadam.
From F`Shangwe
0 Comments