Waziri wa zamani wa fedha wa Urusi, Alexei Kudrin, anasema uchaguzi wa bunge wa mwezi huu ulikuwa na dosari, na nchi inahitaji uchaguzi mwengine ufanywe na ziwepo sheria mpya za uchaguzi.
Alisema wale waliohusika na ulalamishi katika uchaguzi wa karibuni wanafaa kushtakiwa.
Kwa vile yuko karibu na waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin, Bwana Kudrin alikaribishwa kwa mbinja na kelele kutoka kwa maelfu ya waandamanaji katikati ya Moscow.
Maandamano yanafanywa sehemu mbali mbali za Urusi kupinga matokeo rasmi ya uchaguzi huo, ambayo yalikipa ushindi chama cha Bwana Putin.
Katika mji wa Vladivostok, mashariki mwa Urusi, waandamanaji walibeba mabiramu yasemayo kuwa Bwana Putin ashtakiwe.
0 Comments