Mapigano makali yanaendelea katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu huku vikosi vinavyounga mkono serikali ya mpito vikikabiliana na wapiganaji wa al- Shabaab.
Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika nchini Somalia vinahusika katika harakati za kuwasaka wapiganaji hao kufuatia uvamizi wa mara kwa mara wa kuvizia unaotekelezwa na kundi la al-Shabaab.
Wapiganaji hao wanadaiwa kuvamia kituo kimoja kilichoko katika wilaya ya Wadajir inayodhibitiwa na vikosi vya Umoja wa Afrika.
Idadi ya walioathiriwa kwenye mapigano hayo haijulikani kufikia sasa.
CHANZO CHA HABARI
0 Comments