Waziri Mkuu wa Pakistan, Youssef Raza Gilani, anasema nchi yake haiamini Marekani, na Marekani ina hisia kama hizo kuhusu Pakistan.
Bwana Gilani aliiambia BBC kwamba inaweza kuchukua majuma kadha kabla ya Pakistan kuacha kuzuwia misafara ya NATO, kupita mpakani kuingia Afghanistan.
Uhusiano baina ya Marekani na Pakistan uliharibika pale wanajeshi 24 wa Pakistan, walipouliwa na ndege za NATO, katika vituo vya ukaguzi vya mpakani, mwezi uliopita.
0 Comments