Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema kuwa Uingereza itakuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa mwaka ujao litaklojadili kuhusu mzozo wa kivita nchini Somalia na uharamia katika Ghuba ya Aden.
Bwana Cameron amesema kuwa Somalia ni taifa lisilokuwa na utawala thabiti na hivyo linatishia maslahi ya Uingereza wakati wasomali wenyewe wakiteseka kwa njaa na umaskini uliosababishwa na vurugu.Akizungumza mjini London, bwana Cameron amesema kuwa ni sharti pawe na juhudi za kimataifa kuzima shughuli za uharamia pamoja na kushughulikia matatizo ya Somalia.
0 Comments