Mapochopocho yaliyosindikiza sikukuu ya kuzaliwa kwa bwana Hija leo hii,ni Bites za kufa mtu na vitumbua vya mayai ,achilia sambusa zenye nyama ya bata mzinga,Eggs chops za mayai ya tausi na mishikaki ya nyama ya Nyati eeebwana wee tusiokuwepo wacha mate yatutoke, Angalia maandishi yaliyoandikwa toka kwa shemeji kwenda kwa mumewe juu ya keki mmmh wacha weeeeee.
Pichani shekh Hija akipokea Boxes nzuri za zawadi toka kwa mkewe mpenzi mama Laila,mara nyingi inakuwa nadra sana kwa wapenzi kupeana zawadi ila hapo kwa wengine iwe fundisho kuwa zawadi nzuri na tamu itoke kwa mwenzio bwana.
Na wahenga walishasema kwamba mtoto umleavyo na ndivyo akuavyo,kama utafundisha mwanao tabia ya kutoa mapema basi ujue lile neno mkono wa birika litasikika hewani tu,Pichani mwanadada ambaye anatuwakilishia vyema blog hii bi Laila akimkabidhi baba yake mzazi zawadi kama ishara ya upendo kwa siku hii ya kuzaliwa kwa mzazi wake.
TAFAKURI YANGU:KUNANI WANA BIRTHDAY
Sherehe ya siku ya kuzaliwa ni muhimu sana kwa watu wengi japokuwa tupo mwenzangu na mie tunaoona ni siku kama nyingine ambayo imeongeza idadi ya miaka kwa ukamilifu.Wengi huisheherekea kwa kuita ndugu jamaa na marafiki kujumuika pamoja katika sherehe hii.
Kwa wenzetu wanapoisheherekea siku hii kwa kawaida huwa wanataja wametimiza miaka mingapi katika maisha yao tangu kuzaliwa,lakini cha kushangaza sisi tunaoiga utamaduni huu(sio wetu hapo awali)ambao tumeukopa(adapt)kutoka kwa wenzetu huwa hatupendelei kutaja tumetimiza miaka mingapi.Pengine hayo ni maboresho katika utamaduni tulioukopa au sijui kuna kitu gani ambacho kimefichikana hapa? Natumaini wasomaji wenzangu mtamisaidia kwa hilo.
Pamoja na kuwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa na nimependa watu wengi wajue kwa kujitoa kwenye picha hapo juu lakini nimeshindwa kutaja miaka yangu kwa sababu waliotangulia hawakufanya hivyo na mimi nafuata mkumbo na kuogopa kujitia mjuaji mbele ya wengine hali ya kuwa sijui kwa sababu gani wenzangu hawataji miaka yao siku yao ya kuzaliwa.
Kama ingekuwa ni sisi waafrika ambao tunaishi ulaya tu labda ningeweza kuchanganua kutoka akilini mwangu,kwamba ulaya tunatumia vitambulisho ambavyo alama muhimu ni tarehe ya kuzaliwa na juu ya kuwa kila kitu kinapitia kwenye mtandao kwa hiyo inakuwa ni rahisi mtu kupata data zako kwa njia hiyo hali yaku sisi ni wageni(msafiri kafiri)wengi mambo yetu hayako katika mnyoofu kiasi cha kwamba tarehe zetu kamili zinaweza kutuletea matatizo kutokana na unavyojisema mbele za watu na data zako kwenye dola zinavyozungumza,lakini kwa watu wa nyumbani sipati jibu.Labda ni kwamba mtu anaona aibu miaka yake ikijulikana akaonekana mdogo?kwa sababu sisi wabongo tunaupenda ukubwa siku zote na tunapenda tujulikane tuna umri mkubwa kuliko tulivyo ili kulinda heshima ambayo haijulikani hata mwanzo wake?Au pengine ni uamuzi wa mtu binafsi ambao unaambukiza kiasi cha kufanya watu wote tuingie katika mtirirko huo?Na kuna wale wenzangu na mimi ambao tunaofuata mkumbo lakini hatujui sababu halisi iliyofichika.
Nina matumainiwenzangu mtanisaidia juu ya hili suala tata katika kichwa changu,kwani hiyo ni tafakuri yangu.(Na shekh Hija wa Maganga One Blog).
Team nzima ya Maganga One Blog Inachukua fulsa hii fupi kukupongeza kwa siku yako nadhifu ya kuzaliwa Hongera sana shekh wetu kwa kutimiza miaka..... na hii ndio Tafakuri yetu ya leo.Ahsanteni sana.
0 Comments