Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeimarisha vikwazo zaidi dhidi ya nchi ya Eriterea kwa kuendelea kuwaunga mkono wapiganaji wa kiisilamu wa Al-Shabaab nchini Somalia.
Kura ya kuzidisha vikwazo hivyo ilipitishwa baada ya mataifa jirani kutoka Afrika Mashariki kuwasilisha hoja dhidi ya Eriterea ambao wanasema ni hiyo inachangia kuzorotesha usalama wa kanda hiiNchi za kanda ya afrika mashariki zilikuwa zimependekeza vikwazo vyenye uzito dhidi ya Eritrea baada ya ripoti ya umoja wa mataifa kugundua kwamba nchi hiyo imekuwa ikiendelea kuwafadhili wapiganaji wa Al Shabaab na makundi mengine ya kigaidi nchini Somalia.
Nyaraka za mapaema za azimio hilo zilipendekeza hatua kadhaa kuchukuliwa ikiwemo kuharamisha uwekezaji wa kigeni katika sekta ya madini nchini Eritrea na pia kuondoa kodi inayotozwa kwa fedha za kigeni zinazotumwa na raia wa Eriterea wanaoishi ng'ambo .
Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na Urusi pamoja na China ambazo zilisema itawaathiri vibaya raia wasio na hatia ndani ya Eriterea.Katika kura ya mwisho Urusi na Uchina hazikushiriki.Hata hivyo Eritrea imesema azimio hilo halina msingi na imekanusha vikali madai yote dhidi yake.
Maafisa kutoka nchi tano za eneo la afrika mashariki walihutubia kamati ya umoja wa mataifa kwa njia ya video kabla kura hiyo kupigwa, ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi. Ingawa nchi yake imewahi kupigana vita na Eritrea, alisisitiza kuwa azimio hili halijashinikizwa na ugomvi kati ya nchi hizo mbili.
Maafisa kutoka nchi tano za eneo la afrika mashariki walihutubia kamati ya umoja wa mataifa kwa njia ya video kabla kura hiyo kupigwa, ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi. Ingawa nchi yake imewahi kupigana vita na Eritrea, alisisitiza kuwa azimio hili halijashinikizwa na ugomvi kati ya nchi hizo mbili.
Eritrea ilikuwa imewasilisha ombi la kutaka rais wa nchi hiyo aweze kuhutubia kamati hiyo wakati nakala ya mapema ya azimio hiyo ilipotolewa. Lakini mabalozi wamesema kwamba kufuatia upinzani wa marekani , hakualikwa kufanya hivyo hadi mwisho wa wiki jana alipokataa akisema kamati hiyo ilichelewa kumualika.
Azimio hilo linshinikiza nchi zingine ziwe na uangalifu ili kuzuia Eritrea kutumia fedha ili kuzorotesha usalama katika eneo la afrika mashariki. Pia linalaumu Eritrea kwa kupanga kushambulia mkutano wa muungano wa afrika uliofanyika nchini Ethiopia mapema mwaka huu.
0 Comments