Wanachama wa bunge la Ulaya wameishtumu Uingereza kwa ubinafsi na kutozingatia umoja kutokana na hatua yake ya kupinga mpango wa nchi za Ulaya unaonuia kunusuru sarafu ya Euro.
Kiongozi wa kundi kubwa zaidi la kisiasa katika jumuiya ya ulaya amesema haoni tena sababu ya Ulaya kuendelea kuilipa Uingereza mchango wake katika bajeti ya jumuiya hiyo.Hatahivyo baadhi ya wabunge wameitetea Uingereza na wengine wakakosoa mpango huo ambao uliafikiwa na nchi ishirini na sita za jumuiya ya Ulaya.
0 Comments