Rais wa Tunisia, Moncef Marzouki, amesema nchi hiyo haitamuwasilisha kwa mashtaka nchini Libya aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Baghdadi Al-Mahmoudi, bila ya hakikisho kwamba atashtakiwa kwa njia iliyo huru na haki na kwamba atalindwa.
Libya inamsaka Bwana Al-Mahmoudi kwa tuhuma za kutumia vibaya mamlaka.
Akiwa ziarani mjini Tripoli, Moncef Marzouki, alisema ni ''haki ya raia wa Libya kumhukumu'' waziri mkuu wao wa zamani.
Bwana Mahmoudi alikamatwa nchini Tunisia Septemba mwaka uliopita kwa kuingia nchini humo kinyume cha sheria.
Makundi ya kutetea haki za binadamu zimeiomba Tunisia kutomurudisha nyumbani bwana Mahmoundi, yakisema haki zake za kimsingi zitakiukwa.
Katika hotuba yake mjini Tripoli, Bwana Marzouki alisema kuwa watu wa Tunisia walitaka kukakishiwaa kwa 100% kuwa haki inatendeka, na kwamba kutakuwa na mahakama huru, kabla ya bwana Mahmoudi kurudishwa Libya.
0 Comments