Msanii Diamond Platnumz mwenye kofia nyeupe kushoto akiwa na mcheza show wake mapema leo asubuhi kabla ya kuingia kizimbani kujibu mashitaka ya kumshambulia na kuharibu mali za mwandishi wa habari bwana Francis Godwin.
Inasemekana hakimu alimuhukumu kijana Diamond kifungo cha miezi sita au alipe faini ya Tshs 50`000,Diamond alilipa faini hiyo na kuwa huru mahakamani hapo.Watu walijazana mahakamani hapo baadhi yao wanasema kuwa msanii huyo Diamond aliangusha kilio baada ya kuona anakwenda jela miezi 6,ila alipopewa nafasi ya kujitetea alimuomba hakimu kuwa amsamehe na kumpunguzia hadhabu kwani alifanya tukio hilo kwa ghazabu.Hata hivyo inasemekana kwamba mlalamikaji wa kesi hiyo bwana Francis Godwin hakuridhia maamuzi hayo na hivyo anategemea kufanya taratibu za kukata rufaa.
Gari ambalo alitumia msanii Diamond kufika nalo mahakani.
Kushoto ni mdhamini wa msanii Diamond bwana Edo bashir akiwa anajadiliana mambo fulani na mlalamikaji wa keshi hiyo bwana Francis Godwin.
0 Comments