Na Shakoor Jongo AMINI usiamini, mastaa wawili wa tasnia ya filamu nchini, Aunt Ezekiel na mwenzake Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ wamechapana makonde kwa kisa cha kuchekesha.
Hekaheka ya mnyukano huo kwa mujibu wa chanzo chetu makini ilitokea usiku wa kuamkia Jumatano Januari 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Coco Star Club, jijini Dar es Salaam.
MWANZO WA SINEMA
Inaelezwa kwamba, Aunt na Steve kila mmoja na kampani ya washikaji zake walitinga ndani ya ukumbi huo kujivinjari, lakini mdudu wa ugomvi anatajwa kuletwa na ofa ya vinywaji.
“Steve alimwita Anita (mmoja wa wasichana waliokuwa na Aunt) akamuuliza unakunywa nini? Akasema Tikila (aina ya pombe) akamwambia chukua tatu, halafu waulize na wenzako (wadau toka kundi la Aunt) wanakunywa nini?” Chanzo chetu kilieleza.
Maelezo baada ya ofa ya staa huyo fundi wa kuiga sauti za watu, yanaruka mpaka kwenye kipengele cha msanii mwenzake kuinuka na kumkwida shati kuanzisha mtifuano ulioshuhudiwa na watu kibao akiwemo pedeshee mmoja.
INAWEZEKANAJE OFA IWAGOMBANISHE?
Paparazi wetu alipopekua zaidi chini ya kapeti aliibuka na visa kama si chuki ya muda mrefu kati ya wasanii hao inayochochewa na kale ka- ugomvi baina ya Aunt na Kundi la Bongo Movie, kwa maana hiyo ofa ilikuwa chachu ya donge la zamani.
“Kiukweli naweza kusema Aunt ndiyo alinipiga, maana sikumrudishia kwa kuwa siwezi kupigana na mwanamke, tatizo ananichanganya kwenye ugomvi wake na Ray (Msanii Vicent Kigosi), alifunguka Steve.



AUNT ANASEMAJE?
Alipoulizwa, mwanadada huyo anayetamba kunako gemu ya filamu kwa nini ajifunge kibwaya kupambana na msanii mwenzake tena wa kiume kwa kisa cha kitoto, alisema:
“Tangu zamani hatuongei, lakini siku hiyo alikuwa ana fosi tuongee, nilipomkatalia, akaanza matusi na kashfa, nilikasirika, sipendi anitumie kupata umaarufu, asimame kisanii kwa jina lake mwenyewe.