Watu karibu 20 wanahofiwa kufa katika ajali ya mashua iliyozama Lamu, Kenya, Jumapili usiku.
Hadi sasa watu kama 50 wameokolewa au kujinusuru wenyewe kwa kuogelea.

Inahofiwa kuwa meli hiyo ilikuwa imebeba abiria kama 70, ingawa inafikiriwa kuwa ilikuwa imesheheni abiria zaidi ya ile idadi inayoruhusiwa.

Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa miili 7 imepatikana.
Joseph Sigei ambaye ni naibu wa afisa mkuu wa polisi katika eneo la Lamu Magharibi aliiambia BBC kwamba walijaribu kazi za uokozi jana usiku lakini walikuwa waendelee leo asubuhi.
Hata hivyo alisema hafikiri kama wale waliobaki majini kucha watakuwa hai.