kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye akionyesha baadhi ya silaha zilizokuwa zikitumia na jambazi huyo baada ya kuzikamata eneo la Kijenge alipokuwa amezificha jambazi huyo. 
Mmoja wa madakitari katika hospital ya mounti meru akiufanyia uchunguzi mwili wa jambazi huyo picha na joseph ngilisho.
Mganga wa kienyeji Anna Loshirali aliyekuwa amemhifadhi
nyumbani kwake jambazi sugu ,na kumtibu majeraha akiwa chini ya ulinzikwenye gari la polisi baada ya kumtia mbaroni.



Joseph Ngilisho,Arusha
JAMBAZI sugu aliyemuua afisa wa polisi ,Kijanda Mwandu wa jijini Arusha,ameuawa na polisi kwa mganga wa kienyeji wilayani Arumeru alikokuwa amejificha akipatiwa matibabu ya kienyeji kutokana na majeraha mbalimbali ya risasi .
Jambazi huyo Elipokea Kaaya(45) ameuawa juzi majiraya saa 12.45 asubuhi kwa kupigwa risasi na polisi , wakati akijaribu kuwatoroka askari polisi waliokuwa wameizingira nyumba ya mganga wa kienyeji ambaye alikuwa amehifadhi jambazi huyo.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye ,tukio hilo limetokea majira ya asubuhi katika kijiji cha Orarashi,Lengijave wilayani Arumeru ambapo askari polisi walipata taarifa kutoka kwa raia mwema na kuizingira nyumba hiyo tangu majira ya saa 8 usiku.
Alisema ilipotimu saa 12.45 jambazi huyo alikurupuka kutoka ndani ya nyumba hiyo na kuanza kukimbia ,ambapo askari hao walianza kumkimbiza ndipo askari mmoja wapo alipomkamata na kuanza kupambana nae.
Andengenye alifafanua kuwa askari hao walifanikiwa kumpiga risasi ya tumboni, ambapo aliishiwa nguvu na kuanguka chini na kwamba alifariki dunia wakati akiwa njiani akipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Alisema katika tukio hilo askari mmoja mwenye namba E.9912 D/C Wito alijeruhiwa katika mkono wake wa kushoto na jicho la kushoto baada ya jambazi huyo kumng'ata kwa meno na amelazwa katika hospitali ya mount meru kwa akipatiwa matibabu.
Awali kabla ya tukio la kuuawa kwa jambazi huyo,januari 3 mwaka huu jambazi huyo aliwashambulia kwa risasi maofisa wawili wa polisi wakati wakijaribu kukamata nyumbani kwake eneo la shangarai,wilayani Aruemru.
Kamanda Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo jambazi huyo alimpiga risasi askari polisi,Kijanda Mwandu ambaye alifariki dunia ,na kumjeruhi askari,Fausine Mafwele wote wa kituo kiku cha polisi mjini Arusha.
Alisema kuwa baada ya tukio hilo polisi ilifanya msako mkali na januari 6 mwaka huu lilifanikiwa kukamata silaha tatu zilizokuwa zikitumiwa na jambazi huyo zikiwa zimehifadhiwa eneo la Moshono jijiniu Arusha.
Ametaja silaha hizo kuwa ni pamoja na SMG No 1016188011 , risasi kumi na moja,Shortgun Moja yenye Model 88-12GA,risasi nne ambapo zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko mkubwa wa Salphate huku zikiwa zimefichwa katika eneo la vichaka ndani ya eneo hilo la Moshono.
Aidha Andengenye alisema kuwa katika tukio hilo watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi ambapo watu hao walikuwa watendaji kazi na jambazi huyo, ambapo watu hao ni pamoja na mke wa jambazi huyo ambaye ni Agness Silas(40), Joseph Haule(33),Juma Salum(46},pamoja na Dainess Masawe(19).
Katika hatua nyingine mwili wa jambazi huyo baada ya kuuawa ulianikwa siku nzima kama sinema katika uwanja wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mount meru,na kushuhudiwa na umati mkubwa wa wakazi mbalimbali wa jiji la Arusha,ambao walishinda wakiutazama.