Tanzania imepokea msaada wa Sh. billioni 22.8 kutoka Serikali ya Japani, kwa ajili ya kusaidia mradi wa kilimo cha umwagiliaji nchini, ambapo wakulima 33,108 wa zao la mpunga watanufaika na msaada huo.

Akipokea msaada huo jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhani Khijjah, aliishukuru Japan kwa msaada huo na kusema kuwa itainua sekta ya kilimo nchini hasa zao la mpunga
 
Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo, na tunaishukuru Serikali ya Japani kwa msaada wake wa kijamii na kiuchumi wanaoendelea kutuaidia,” alisema Khijjah.
Aliongeza kuwa mradi huo utahusisha kilimo cha mpunga nchini katika mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro na Mtwara kwa kufanya tafiti zaidi katika pamoja na wakulima wa zao hilo kuwawezesha kuzalisha kwa wingi hilo pasipo kutegemea mvua.
 
Aidha, alisema fedha hizo zitatumika katika tafiti za kupata mbegu bora la zao la mpunga. Fedha hizo zitaumika kusaidia kituo cha mafunzo ya kilimo cha Kilimanjaro kwa kushirikia na wataaramu kuendesha mafunzo juu ya kilimo cha mpunga, na kutoa elimu juu ya usimamizi wa fedha kituoni hapo.
Pia, zitasaidia katika kutoa mafunzo ya zao la mpunga katika kituo cha MATI-Igurusi mkoani Mbeya na kutoa pembejeo za kilimo zitakazotumika katika kilimo cha zao la mpunga katika kituo hicho.
Tanzania inatarajia kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga kwa mwaka huu kutoka tani 5 kwa ekari moja ilizokuwa ikipata mwaka 2010 hadi kufikia tani sita.