Pichani Jessica Buchanan na Poul Tisted waliokolewa na vikosi maalum vya Marekani.
Vikosi maalum vya Marekani viliingia nchini Somalia usiku wa manane na kufanikiwa kuwaokoa wafanyakazi wawili wa mashairika ya misaada kutoka mikononi mwa watekaji nyara wao nchini Somalia.
Mateka hao, Mmarekani mmoja na raia mmoja wa Denmark walitekwa nyara na kikundi cha Wasomalia mwaka uliopita na kwa mujibu wa tume ya Baraza la Denmark linalohusika na wakimbizi limethibitisha kua Mmarekani Jessica Buchanan na Poul Hagen kutoka Denmark wameachiliwa na wako njiani kujiunga na familia zao.Operesheni hii ilikua ya kipekee na ilibidi kua kivutio kikubwa kwa sababu kadhaa. Kwanza, ni namna ya ujasiri uliotumiwa kuifanikisha. Ni bayana kwamba ufanisi wake utamfaidisha Rais Obama mwenyewe na utawala wake na pia vikosi vya Marekani.
Pia ni kumbusho kua vikosi vya Marekani havijathubutu kuweka guu nchini Somalia tangu kisa cha mjini Mogadishu cha mwaka 1993, ambapo askari 28 waliuawa.
Hata hivyo kumekuwepo matukio ya kutumia makombora ya mbali kuweza kufikia malengo ya vikosi hivyo pamoja na ndege zinazopaa bila rubani kutimiza mashambulizi yanayohitajika.
Na Somalia imezidi kutazamwa kwa mashaka na Marekani pamoja na Mataifa mengine ya Dunia.
Jinsi Operesheni hii ilivyoendeshwa kuwaokoa mateka kutoka mikononi mwa kikundi cha wahalifu ni ishara ya wasiwasi unaozidi kuongezeka juu ya hali ya mambo nchini Somalia na kiwango cha uhalifu kinachozidi kupanda, ikizingatiwa kua kuna utekaji nyara wa Meli baharini na vilevile raia wa nchi za magharibi.
Pamoja na hayo, Marekani imezidisha ukaguzi wa anga ya nchi hio pamoaja na kua na ushirikiano wa karibu na Mataifa jirani kutokana na hofu kubwa juu ya uwezekano wa shughuli zinazokisiwa kua za kigaidi nchini humo.
Hisia mbalimbali zimejitokeza kuhusu shambulio la hivi sasa. Lakini huenda limefanyika kwa sababu Marekani ina uwezo wa kufanya hivyo au kwa sababu uchunguzi wa jasasusi wao umewapa taarifa za kutosha kutimiza operesheni hio.
Huenda likawa tukio la mara moja. Lakini kwa hali yoyote ile, linatimiza haja ya Rais Obama ya kutuma vikosi vyenye uwezo wa kuzima tukio kama hili mara moja badala ya vita vya mda mrefu na kuhitaji askari wengi na gharama kubwa.
Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden akizungumza kuhusu Operesheni hii amesema,Nathibitisha kua Rais mwenyewe ndiye aliyeamuru lifanyike hili. Hakutaka kutoa maelezo zaidi ila tu kusema anazidi kushangazwa na jinsi vikosi vyao vinavyotekeleza operesheni ngumu kama hizo kwa mda mfupi.
0 Comments