Habari za leo wapenzi na wasomaji wa Maganga One Blog.
Tunashukuru tumeuanza mwaka vyema.kwa waliopoteza maisha tunawaombea kwa MUNGU awapumzishe mahala pema peponi Amen.kwa wale waliokuwa wagonjwa nao kadhalika tunawaombea wapone kwa haraka na warudie hali zao kama hapo awali.
JAMBO LA MUHIMU NA KILA MMOJA ALIELEWE
Maganga One Blog ni Blog yenye kukuletea habari za Kitaifa,Kimataifa Burudani na Michezo kwa lugha mbili tofauti,yani Kiswahili na Kiingereza.Blog hii imeanzishwa kimataifa na si kitaifa pekee wasomaji wetu kama mnavyosoma habari zetu.
Habari nyingi sana tumekuwa tukiwaletea kwa lugha ya Kiswahili kwa kuwa wasomaji wengi ni wenye kuifahamu vizuri lugha hii.sio wote wenye kuelewa kiswahili vizuri na sio wote wenye kuelewa kiingereza vizuri na ndio maana tukaweka lugha ya Kiswahili itumike sana kwa wasomaji na kiingereza kitakuwa kikigusiwagusiwa tu kwa mbali na sio siku zote.
Kabla ya hapo tulikuwa tukitumia lugha moja tu ya Kiswahili kuwaletea habari,ila kwa kuwa wasomaji toka nchi za jirani kama Kenya,Uganda,Afrika kusini,zimbabwe,Canada,Holland,Marekani na kwengineko duniani waliomba kuwa baadhi ya habari zingine wangependa ziandikwe kwa lugha ya kiingereza, basi ikabidi ziletwe kama zinavyosomeka.
Kingine ni kwamba kuna habari ambazo zinaletwa kama zilivyo nasi tunazitoa kama zilivyo,kuna habari ambazo hazihitaji marekebisho kutokana na sababu za msingi na kazi za tasnia hii ya habari basi nasi hufanya na kufuata sheria na kanuni za kazi hii.Kuna kitu kinaitwa haki miliki,ukipundua habari ya mtu na kuifanya unavyotaka wewe,sheria inakupinga na unaweza kujikuta unaharibu badala ya kutengeneza.
Hivyo basi,nawaomba sana wapenzi wangu wote wa Maganga One Blog,kuivumilia hii hali,kwani hata mimi napenda sana kuwaridhisha mnavyotaka ila inakuwa ngumu kwa upande wa kugeuza baadhi ya habari na kuondosha ladha halisia ya habari hiyo.Tunajitahidi baadhi ya habari kuzigeuza na kuwa kwa lugha ya Kiswahili ila kuna habari inabidi zisomeke kama zilivyo.kwani kuna habari zingine tunaletewa na kuna habari zingine ni uchambuzi wa magazeti.
Nategemea kila mmoja wetu atakuwa amenielewa na atakubaliana na ufafanuzi wetu juu ya suala la habari za kizungu.nawaomba sana mnielewe kwa hilo kwani nikipindisha sheria,sheria itaninyoosha ndugu zangu.kumbukeni blog zinafuta taratibu na sheria zote za uhandishi.hata ukichukua habari sehemu ni lazima useme hii habari imetoka wapi.
Mwenye maoni,ushauri zaidi tunamkaribisha kwa moyo mweupee,na tunashukuru sana kwa maoni yenu juu ya suala la lugha.tunafurahi kila mnaposema yanayowakera,tunashukuru kuwa nasi bega kwa bega kila siku nawaahidi bado nalishughulikia suala hili.ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu.
Maganga One team.
0 Comments