Kutoka kushoto ni Rashid Matumla ambaye miaka ya nyuma alililetea taifa la Tanzania jina kubwa katika medani ya mchezo wa ngumi.anayefuata ni mtoto wa Rashid Matumla ambaye ni Mohammed Matumla,mwenye taulo mabegani ni Mbwana Matumla kadhalika ametuweka watanzania katika ramani na kiwango cha juu duniani katika mchezo wa ngumi.wa mwisho ni Mkwanda Matumla ambaye nae ni moto katika mchezo huo.sio hawa tu wapo wengi mpaka dada zao wanapigana ngumi.Rashid Matumla na Mbwana Matumla wameshawahi kuwa mabingwa wa dunia katika mchezo huu miaka ya nyuma.Taifa liwaangalie watu kama hawa na kuwathamini kwa mchango wao wa Taifa.