Ripoti kutoka Italia zinasema kuwa watu wasiopungua sita wameuwawa baada ya meli kubwa ya abiria kuanza kuzama karibu na pwani ya magaribi mwa taifa hilo na kuanza kujaa maji.
Abiria walisema kuwa walisikia sauti kubwa kabla ya meli hiyo kusimama na taa zote kuzima wakati ilipoanza kuzama. Ishara ya kuondoka kwenye meli ilitolewa na baadhi ya abiria waliruka nje na kuogelea hadi ufuoni.
Wengi wa abiria hao alfu nne na ishirini wameondolewa kwenye meli hiyo, kwa jina Costa Concodia ambayo ilikuwa ikizuru bahari ya Mediterranean.
Helikopta zilitumwa kuwaokoa watu ambao bado wamekwama ndani ya chombo hicho.