Rais Jacob Zuma akihutubia umma.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amehutubia maelfu ya wafuasi wa ANC, katika sherehe zinazomalizika leo(jana) za kuadhimisha miaka 100 tangu chama hicho kuundwa - chama kikongwe kabisa cha ukombozi barani Afrika.
Umati wa wanasouth Afrika ukisikiliza kwa makini hotuba mbalimbali uwanjani hapo.Bwana Zuma alisema leo(jana) ni siku ya furaha kwa watu wa Afrika Kusini, ambao waliangamiza ukoloni na ubaguzi wa rangi, kwa kusaidiwa na Afrika na ulimwengu.
Bwana Nelson Mandela hakuweza kuhudhuria kwa sababu ni dhaifu.
Rais Jacb Zuma alipokuwa akiondoka uwanjani hapo
ANC hivi karibuni imekumbwa na kashfa za rushwa na mizozo ndani ya chama lakini bado kina wafuasi wengi
Kati ya wageni waliohudhuria sherehe hizo ni Kasisi Jesse Jackson, mwanaharakati maarufu wa Marekani wa kutetea haki za weusi.
Alisema: "Baada ya karne moja - kutoka madhalilisho, kachomoza Nelson Mandela, Thabo Mbeki, Jacob Zuma, na Barack Obama.
Ni karne ya mifano ya kuvuka vizingiti vikubwa.
Na khofu waliyokuwa nayo wazungu - kwamba weusi watalipiza kisasi - hayakutokea hayo".



1 Comments
for allowing for me to comment!
my site > Games New