Na Mwandishi Wetu
MZEE mmoja kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinaswa kitandani ndani ya chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar, Amani linasasambua.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kyando, anasemekana amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa Fatty kwa siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya majirani wa nyumbani kwa msichana huyo.
Mpashaji wetu akasema kuwa katika kufunuafunua ukaribu wa msichana huyo na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa wawili hao wana ukaribu usiofaa.
SIRI YAVUJA
Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo mpenda kukaa na watoto wa wenzake.
“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba, alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani, kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.



MTEGO WAFYATUKA, WANASA
Mashuhuda wa sakata hilo waliliambia Amani kuwa mama mdogo na watu wengine waliwanasa wawili hao wakiwa juu ya kitanda kama walivyozaliwa, bila kufafanua walichokuwa wakikifanya.
Mtoa habari wetu alisema kuwa ili kushika ushahidi mkononi, mama mdogo wa binti huyo na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video kisha wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye inaaminika ni mume wa mtu.Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana kwao.
Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni kulilipwa fedha nyingi.

KISA CHA KUJUANA
Habari nyingine zinadai kuwa wawili hao walifahamiana miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo ‘mshitakiwa’ alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini Dar.

KIGOGO AKOROMA KWENYE SIMU
Namba ya simu ya mfanyabiashara huyo ilipatikana hewani Jumatatu iliyopita na aliposomewa mashitaka yake, alikuja juu kama moto wa gesi huku akitishia kumfikisha mtu kwenye kizimba cha mbao anazouza, yaani mahakamani kama siyo kortini.
 
GPL