Na Brighton Masalu
STAA mwenye jina kubwa Bongo, Steven Kanumba (pichani), amejitoa katika klabu ya wasanii wa filamu ya Bongo Movie, Risasi Mchanganyiko linaripoti kifua mbele.
Chanzo chetu ndani ya klabu hiyo, kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, kinaeleza kuwa Kanumba amefikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na mambo yasiyoeleweka ndani ya klabu hiyo.
“Jamaa (Kanumba) amejitoa muda mrefu sana, ila hivi juzi ndiyo imethibitika baada ya kuonekana anajitenga katika shughuli za klabu.
“ Tangu kufukuta kwa bifu lake na Ray, hajawahi kuhudhuria vikao vya klabu yetu wala sherehe za wasanii wenzetu isipokuwa ya kuzaliwa kwa Irene Uwoya ambapo hata hivyo, hakuwa karibu na memba wa Bongo Movie.

Anasema hakuna ishu, ni kupotezeana muda na kutiana umaskini tu,” alisema.
KANUMBA ANAFUNGUKA
Baada ya kuweka kibindoni madai hayo, gazeti hili liliwasiliana na Kanumba na kumweleza kuhusu madai hayo ambapo alishindwa kukubali wala kukataa.
“Tatizo kwa sasa nipo busy na kazi zangu... kuhusu Bongo Movie ni kweli sijakaa nao muda mrefu, suala la kujitoa linabaki kuwa binafsi. Tuliache kwanza kwa sasa, lina upana wake.”
JB ANASEMAJE?
“Hata mimi nimesikia hayo maneno ila Kanumba hajaniambia wala kuniandikia barua. Akinithibitishia kwa barua, nitaamini hizo fununu, lakini kwa sasa bado namhesabu kama mmoja wa wanachana wangu.”