TANZIA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepatwa na majonzi makubwa na kinasikitika sana kwa kifo cha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Taifa, Mheshimiwa Regia Mtemaambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum na Waziri Kivuli wa Kazi na Ajira.  MheshimiwaRegia Mtema amefariki leo tarehe 14 Januari 2011 kwa ajali ya gari katika eneola Ruvu darajani.


Katika uhai wake marehemu Regia Mtema amefanya kazimbalimbali za kisiasa na kijamii katika taifa. Marehemu Regia Mtema amezaliwatarehe 21 mwezi Aprili mwaka 1980 na kusoma shule za sekondari kidato chakwanza mpaka cha sita katika shule ya sekondari ya Forodhani na Shule yaWasichana ya Sekondari ya Machame. Marehemu Regia Mtema alipata shahada yake yakwanza (Bsc Home Economics and Human Nutrition) katika Chuo Kikuu cha Kilimocha Sokoine.


Mara baada ya kuhitimu masomo yake marehemu Regia Mtemaalifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na CHADEMA nakuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA nabaadaye kuteuliwa kuwa Afisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya CHADEMAnafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa mbunge wa vitimaalum.


Viongozi wakuu wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti FreemanMbowe ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Katibu Mkuu Dr.Wilbroad Slaa, wajumbe wa kamati kuu, wakurugenzi wa chama makao makuu na wabunge wamejumuika hivi sasa na familia ya marehemu katika kipindi hikikigumu.


CHADEMA inatoa pole kwa familia ya marehemu Regia Mtema,wanachama wote na wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususani wa Jimbo la Kilomberokutokana na msiba huu wa ghafla katika wakati ambapo mchango wake ukihitajikakwa chama na kwa taifa.


Taarifa zaidi kuhusu taratibu za maziko, itatolewa mara baadaya kukamilisha majadiliano baina ya familia ya marehemu, chama na Ofisi yaBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mipango ya mazishi ya marehemu inapangwa nyumbani kwa Baba wa Marehemu Regia Mtema, Ndugu Estelatus Mtema, Tabata Chang'ombe. Ratiba ya maziko itatolewa baada ya kukamilika kwa taratibu zinazopangwa na familia ya marehemu, Ofisi ya Bunge na chama.


Mungu ailaze roho ya Marehemu Regia Mtema, mahali pema peponi. Amina.




Imetolewana:


JohnMnyika(Mb)


Mkurugenzi wa Habari na Uenezi