Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na rais wa PST, Emmanuel Mlundwa yenye namba VP/2012/1, bodi ya PST iliamua kumsimamisha Mnazareth kuendelea kuwa makamu wake wa rais hadi pale uchunguzi utakapokamilika.
PST iliamua kumsimamisha kufuatia kumtuhumu Mnazareth kuwa match maker wa pambano la Nyirawila na Cheka huku akielewa kufanya hivyo kumeigharimu nchi kupoteza mkanda WBF aliovuliwa Nyirawila.
“Tumemsimamisha na sasa yuko katika uchunguzi endapo tutagundua anahusika katika hilo hatutakuwa tayari kufanya naye kazi hivyo atakuwa amejiondoa moja kwa moja PST," alisema Mlundwa.
Hata hivyo, Mnazareth alisema yeye aliamua kumsaidia Philemon Kyando ambaye ndiyo muandaaji wa pambano hilo kutafuta mabondia ambao watachuana hadi kuwapata Cheka na Nyirawila.
Alisema yeye ni 'match maker', na kufanya hivyo ni kazi yake na kusisitiza hata Mlundwa ni 'match maker' nje ya nchi hivyo yuko tayari kwa maamuzi yoyote.
0 Comments