Thierry Henry akimchagua kipa wa Leeds United na kuandika bao la kwanza na la ushindi kwa timu yake ya zamani ya Arsenal.goli pekee la Henry limeifanya timu ya Arsenal kusonga mbele katika mashindano ya FA nchini Uingereza.
Thierry Henry akishangilia kwa furaha zote goli lake la jana kwa mashabiki wake wa zamani wa timu hiyo,Henry yupo Arsenal kwa mkopo wa miezi miwili.
Hapo Henry kamfuata kocha wake na kumkumbatia kwa furaha kwa kuifungia timu yake goli hilo.

Thierry Henry amerejea Arsenal kwa kishindo na kuisaidia timu hiyo kusonga mbele katika michuano ya Kombe la FA baada ya kufunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Leeds United.
Arsenal wamesonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0.
Henry, 34, alifunga goli lake la 227 kwa Arsenal baada ya kurejea kuichezea klabu hiyo kwa mkopo wa miezi miwili.
Arsenal sasa itakutana na Aston Villa katika raundi ya nne ya kombe la FA katika mchezo utakaochezwa Januari 28