Nikiwa nchini Holland nilibahatika kuinasa hii picha ambayo inaonyesha mimea ya Bangi ikiwa imestawi vizuri kwenye moja ya jengo la mkazi mmoja jijini hapo.Tofauti na nchini kwetu au Afrika kwa ujumla kwamba uvutaji wa bangi si ruhusa ila kwa nchi ya Holland na baadhi ya nchi za ulaya zinaruhusu uvutaji wa bangi.Nimeshuhudia baadhi ya vijana hata watu wazima njiani wakiwa wameshikilia vipisi vya bangi huku wavuta bila wasiwasi wowote.Kinachokatazwa ni kwamba usikamatwe na kiwango kikubwa cha kilevi hicho.