Kuna baba mmoja wa Kichaga ambaye alikuwa akiteka maji kisimani kwa bahati mbaya alikanyaga vibaya ukingo wa kisima na kudumbukia kisimani.

Alipiga kelele sana ili watu waje kumuokoa,kwa kuwa alikuwa akiishi karibu na nyumbani kwake mkewe alisikia zile kelele za mumewe,mkewe alikimbilia mbio kisimani na kukuta mumewe katumbukia ndani ya kisima.mambo yakawa kama ifutavyo:-

Mume- Jamani nakufaaa,niokoeni jamani niokoeni nakufa mieeee

Mkewe - Oooh mume wangu jamani (huku akilia sana mikono kichwani)

Mume- Mke wangu niokoe jamani nakufa mieee

Mke- acha nikanunue kamba nakuja mume wangu

Mke akakimbilia dukani kununua kamba na kurudi na kamba ndefu ya mkonge.
alipofika kisimani mambo yakawa kama ifuatavyo:-

Mke -Mume wangu daka kamba hiyo mie nakuvuta juu sawa?

Mume- sawa mke wangu

Mke- shika vizuri muwe wangu
Yule mume alipoishika ile kamba vizuri na kuiangalia akaona ni kamba mpya kabisa,akili haikumpa na akahoji kama ifuatavyo:-

Mume- Mke wangu aithee hii kamba ni mpyaa eehe?

Mke - Ndio mume wangu ni mpya

Mume - Umenunua kiathi gani aithee?

Mke - Nimenunua elfu 1000 kwa mzee Bizo

Mume- Hapana,mama Manka,please rudisha hii kamba,rudisha haraka kwani bei ni kubwa sana nenda kanunue lile duka la Mshihiri pale kona ni mia 500 tu aithee.


Waungwana kwa kukuonesha jinsi kabila la Wachaga walivyo wabahili mpaka kifo chake mtu anakikubali kwa 500 tu.

Mie mbavuu sina jamani.
              (Na Sharobaro Chura wa Holland)