Ni tope zito lenye harufu mbaya katikati ya barabara huku watu wakifanya biashara zao kama hawaoni na kujali afya zao.
Wafanyabiashara wadogowadogo wakiendelea na biashara zao kama kawaida huku mbele yao na nyuma yao kukiwa na uchafu ambao wameufumbia macho.Wananchi hawa wanachangishwa kodi ila wizara husika sijui inawajibika vipi juu ya hilo.
Biashara ya silaha barabarani,wafanyabiashara pande zote mbili,wapita njia nao wanapita kwa shida kabisa kwenye uchafu uliotanda barabarani mjini Arusha.
Kwa mji mkubwa kama Arusha na Utalii tunaojivunia toka kwa raia wa kigeni wanapotembelea sehemu kama hizo ni aibu sana kwa taifa letu.wananchi wanalipa kodi ila hazifanyiwi kazi ipasavyo.
Jionee mwenyewe bila hata kusimuliwa,hali kama hii watu wakiumwa kipindupindu ni nani wa kulaumiwa? ewe kiongozi uliyepata kura ya mwananchi wako fanya jitihada za ziada kuinusuru hali hii kwa wananchi wako,au kila kitu mpaka afanye rais?(picha zote na Daniel wa Maganga One Blog).
0 Comments