Kamishna Msaidizi wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati na Madini Bw, Prosper Victus (alisimama mbele na Kabrasha) akitoa maelezo ya awali wakati wa uwekaji wa saini mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jana wakati wa hafla hiyo kwenye jengo la Wizara ya hiyo jijiji Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TDPC Bw, Yona Killagane akitoa maelezo mafupi Jan 24,2012 kabla ya kusain i mkataba wa utafiti wa mafuta nchini utaozishirikisha kampuni tatu kutoka nje, Kampuni hizo ni Petrobras, Heritage na Motherland Industries Limited.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kulia) akifafanua jambo wakati wa uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uatafiti wa mafuta kutoka kampuni za nje jijini jana DSM (Kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Nishati (Petroleum na Gas ) Bw, Prosper Victus.
Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (katikati) akiweka saini mkataba wa utafiti wa mafuta nchini kwa kampuni tatu kutoka nje, (kushoto) ni Mkurugenzi mtendaji wa TPDC Bw, Yona Killagane na (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Matherland industries LTD kutoka India, Bw. V.K. Sood .(kulia). Mkataba huo umewekwa saini  jana  kwenye jingo la Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) akibadilisha hati za makubaliano ya utafiti wa mafuta nchini na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia) , hafla hiyo imefanyika jana  jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje.
Waziri wa Nishati na Madini Wiliam Ngeleja (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampun i ya Petrobras kutoka Brazil Bw, Samuel Bastos de Miranda (kulia),wakionyesha mikataba waliyoisaini wakati wa hafla hiyo iiliyofanyika jana jijini Dar es Slaam wakati wa hafla ya uwekaji saini wa mikataba mitatu ya utafiti wa mafuta wa kampuni kutoka nje.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).