Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Australia ameonya kuwa Ulaya imeshughulishwa mno na matatizo yake ya kiuchumi, hata inakosa kushiriki kwenye mjadala kuhusu kukuwa kwa taifa la Uchina na sehemu nyengine za bara la Asia.
Akizungumza katika mkutano kuhusu usalama unaofanywa mjini Munich, Ujerumani, Kevin Rudd alionya kwamba Ulaya ikiendelea kuzungumza sana, kuna hatari kuwa itauwa mapema uchumi na siasa zake.
Tamko la Bwana Rudd lilitolewa maanani na afisa wa Umoja wa Ulaya anayeshughulika na masoko, Michel Barnier, ambaye alisema Ulaya itaibuka na nguvu na uongozi bora zaidi kutokana na msuko-suko wa hivi sasa.
0 Comments