Habari za jumamosi waungwana wote popote duniani.
Wiki hii tumekuwa na hali ya hewa ya baridi sana kiasi kwamba kuna baadhi ya watu wanapozea maisha kutokana na hali hii ya baridi kali.

Kinyume na matarajio ya wengi,binafsi nimekuwa mtu wa ajabu kulingana na wengi wa wenzangu tunaoishi huku Nzega.wengi wakiwa wametokea Afrika wakija huku na kukutana na hali ya hewa ya baridi kali sana hufikia wakati wanasema ``tunajuta kwanini tumekuja huku``mimi huwashangaa sana kutokana na kauli za wengi wao wanapokuwa kule Afrika,wengi wao walipokuwa Afrika walifikia kipindi wakikufuru Mungu kwa kusema ni ``heri kuzaliwa paka ulaya kuliko kuwa mwanadamu Afrika``na wengine hulalamika sana kutokana na hali ya joto la Afrika na kusema ``ni bora kufa na baridi ulaya kuliko kuishi kwenye nchini yenye joto na moto kama hii``.

Binaadamu tumekuwa tukijisahau sana na kauli zetu na na kufikia kukufuru MUNGU kwa kutoridhika na hali ya maisha na mazingira tuliyokuwa nayo.Umekimbia Joto kwenu na kufuata Baridi kwenye nchini ya wenzako,matokeo yake unalalamika kwamba huwezi kuishi katika hali ya baridi kali,sasa ukiwa umekimbia hali ya Joto kali na kuja kwenye baridi kali    utaweza kuishi mahala gani wewe?

Nawaomba wanaadamu wenzangu tuwe na shukrani kwa MUNGU kwa hali na mazingira tunayokutana nayo kila siku za maisha yetu.Pichani leo ndio tumeamka hivyo,Ahsanteni nawatakia jumamosi njema.
                              Maganga One -Blogger.