Gladness Mallya na Issa Mnally
SIKU chache baada ya Maimartha Jesse kufunga ndoa ya siri na mchumba’ke aliyetajwa kwa jina moja la Shaa, amefanya kituko cha mwaka kwa kubadili utaratibu uliozoeleka wa kufanya sherehe ya send-off baada ya harusi.
Mai ambaye ni mtangazaji maarufu Bongo aliangusha pati hiyo ya kuagwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mastaa wa filamu na muziki.
Katika tukio hilo lililohudhuriwa na timu yetu, baadhi ya waalikwa walisikika: “Hii ya Mai kiboko, sisi tumezoea kufanya send-off ndiyo harusi inafuata, lakini hii ni ya aina yake.”
Ishu nyingine iliyoibua minong’ono ni kitendo cha Mai kutakiwa kumkaribisha mumewe chakula ambapo mshehereshaji Epharaim Kibonde alimwambia amlete mwandani wake, lakini staa huyo akaenda kumshika mkono shemeji yake badala ya mhusika.
Katika nusanusa ya Ijumaa Wikienda, ilidaiwa kuwa mwanaume huyo hatakiwi kuonekana kutokana na kazi yake (haikutajwa), jambo lililoongeza maswali na kuonekana kituko.
Februari Mosi, mwaka huu, Mai alifunga ndoa ya siri na Shaa katika Kanisa Katoliki Kigamboni, Dar na kuhudhuriwa na watu wachache ambao ni ndugu tu.
0 Comments