Na Issa Mnally
NI kimbembe! Yule mwanamke aliyenaswa na askari wa Kituo cha Polisi Magomeni, jijini Dar katika nyumba moja ya kulala wageni na mwanaume ambaye ni Raia wa Bangladesh, amepigwa talaka na mumewe ambaye jina lake halikutajwa.
Risasi Mchanganyiko pekee ndilo lenye mkoba wenye kila kinachohusu ishu hiyo na hapa linakudondoshea bila woga wala wasiwasi, tambaa na mistari katika para zinazofuata.

KUMBE NI NESI!
Akizungumza na gazeti hili, shemeji wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ally Abeid, alisema shemeji yake huyo ni nesi katika Zahanati moja iliyopo jijini Dar es Salaam.
“Shemeji ni nesi, tena analipwa vizuri tu, wakati mume wake ni mfanyabiashara ambaye anasafiri kila mara kikazi. Nahisi ndiyo maana alitumia upenyo huyo kumsaliti ndugu yetu.




ISHU MEZANI
Akizungumza kwa masikito makubwa, Ally alisema kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko katika ndoa ya shemeji yake na kaka yake, kuhusu uaminifu lakini mwanamke huyo amekuwa akiruka vikali.
Akiendelea kuweka mambo hadharani, Ally alisema kwa sasa kaka yake yupo safarini Shinyanga kikazi, hivyo wakati tukio hilo linatokea hakuwepo.
“Kwa sasa kaka yupo Shinyanga kikazi, lakini ni muda mrefu sana shemeji amekuwa akilalamikiwa kutokuwa muaminifu, lakini amekuwa akikataa katakata. Kaka amejitahidi kumuwekea mitego mingi bila mafanikio.
“Juzi hapa ndiyo tukashangaa tunamuona kwenye gazeti akiwa na yule mzungu (Mbangladesh), tukaamua kumpigia na kumweleza juu ya habari hizo, hakuamini hadi aliponunua Gazeti la Ijumaa na kujionea mwenyewe,” alisema.
Alisema kaka yake baada ya kupata uhakika wa habari hizo, aliamua kuandika talaka akiwa huko huko Shinyanga na kuituma Dar es Salaam ambapo waliipokea na kumpa shemeji yao.
“Tulichokifanya sisi kama ndugu, hasa wa kiume, tulimpatia shemeji talaka yake na kumuamuru aondoke nyumbani kwa kaka yetu kwa kuwa si mwaminifu,” alisema.
Juhudi za kumpata mwanamke huyo hazikuzaa matunda baada ya simu yake iliyotolewa na shemeji yake kutokupokelewa muda wote ilipopigwa.

TUJIKUMBUSHE
Habari ya mwanamke huyo kunaswa akiwa na mwanaume huyo wa Kibangladesh, iliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti ndugu moja na hili, Ijumaa katika toleo la Ijumaa iliyopita Fabruari 3, 2012 namba 759 lililokuwa na kichwa cha habari KUDAADEKI.
Habari zilizopatikana eneo la tukio, wakati kashkash hiyo ikiendelea, zilinong’ona kwamba mwanamke huyo ni mke wa mtu, jambo ambalo limedhihirika baada ya shemeji yake kuibuka na kuanika ukweli huo.

                                                                 chanzo