Javier Hernandez au unaweza kumuita Chicharito akipiga mkwaju mkali wa penati ambao ulimshinda mlinda mlango wa Stoke City na kuandika bao la kwanza kwa Manchester United.
Safii kijana,safi sana ebu gonga kwanza..hapo ni Rio Ferdinand kushoto akimwambia kijana wake Chicharito baada ya kutingisha nyavu kwa njia ya penati.
Aaah mambo gani tena ya kusukumana eneo la hatari? hapo mchezaji wa Manchester united Valencia anaonekana akilalamika kwa refa baada ya mchezaji wa Stoke City Walter kumsukuma eneo la hatari,refa hakuona uvivu kutoa penati nyingine kwa Manchester united na matokeo yake angalia picha ya chini.
Ni kijana mzuri kwa ufungaji wa magoli kwa Manchester united,anakwenda kwa jina la Dimitar Berbatov akiweka mpira kwenye nyavu na kuandika bao la pili kwa Manchester United,mpaka mwisho wa mpira Manchester United 2-0 Stoke City.

Haya ni matokeo kwa mechi za jana ligi kuu nchini uingereza
FTSwansea City1-1ChelseaLiberty Stadium (20,526)
FTTottenham Hotspur3-1Wigan AthleticWhite Hart Lane (35,801)
FTWolverhampton Wanderers0-3LiverpoolMolineux Stadium (27,447)
FTEverton1-0Manchester CityGoodison Park (29,856)
FTManchester United2-0Stoke CityOld Trafford (74,719