Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kulia) akitoa maelekezo yaliyopo katika fomu ya uthibitisho wa ushindi kwa mshindi wa shilingi milioni 50 wa droo ya pili ya promosheni ya Mzuka wa Airtel Bi Hadija Omary Issa kabla ya kusaini fomu hizo jana katika ofisi za Airtel Makao Makuu . Hadija atakabithiwa pesa zake taslimu katika wiki chache zijazo.
 
Mshindi wa pili wa shilingi milioni 50 wa promosheni ya Mzuka wa Airtel Bi, Hadija Omary Issa (kushoto) akisaini fomu ya uthibitisho wa malipo ya fedha zake baada ya kuibuka mshindi wa pili wa promosheni hiyo ambayo inaendelea kwa wateja wote wa Airtel Tanzania, anayeshuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde wakati wa hafla fupi iliyofanyika jana katika ofisi kuu za Airtel Tanzania.