Na Mwandishi Wetu.

KLABU ya Bongo Movie, ilitajwa kuwa kiunganishi cha wasanii hai wa filamu katika kusaka mafanikio na kujitolea kufanya kazi za kijamii, lakini yameibuka madai kuwa muunganiko huo hauna tofauti na danguro.
Madai hayo yamemenywa na kubaki kuwa maudhui yanayotajwa kuunda kundi hilo ni danganya toto.
Vyanzo visivyo na shaka vimedondosha nyeupe kuwa uchafu unaofanywa na baadhi ya mastaa wanaounda Bongo Movie, hauna tofauti na vitendo vya danguro.
Baadhi ya wasanii wanaounda klabu hiyo wanadaiwa kuzungukana wao kwa wao kimapenzi.
“Mimi nimekataa kabisa, pale Bongo Movie ni kama nipo au sipo, hawanishirikishi kwenye mambo yao,” alisema msanii mmoja wa kiume kwa sharti la kutotajwa jina.
Aliendelea: “Mapenzi yanachukua nafasi kubwa pale. Niliwahi kuanza uhusiano na msanii mmoja, tukashiriki tendo, ghafla jamaa mwingine naye akamchukua. Mimi nikaona kinyaa, nikaachana naye.
“Huwezi kuamini mpaka sasa msanii huyo wa kike ameshatembea na wanaume wanne, watu hawana aibu hata kidogo. Wapo wasanii wa kiume pale wameshatembea karibu na mabinti wote.“Kuna watu wana wake zao lakini wanafanya mambo ya kushangaza.


Fuatilia utagundua, wanaume ambao siyo wasanii, wengi wameachana na wapenzi wao kwa sababu ya hali halisi. Mtu ana mume wake, akifika Bongo Movie anaanza kutoka na wasanii wenzake, mume hawezi kukubali, anabwaga manyanga.”
Wakati hayo yakisemwa, ilidaiwa kwamba ugomvi wa maastaa wawili, Steven Kanumba na Aunt Ezekiel, chanzo chake ni mapenzi, kwani walianza tabia ya kuoneana wivu ndani ya klabu.
Ilinyetishwa kuwa vitendo vya ufuska ndani ya Bongo Movie, hutekelezwa zaidi usiku, Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam.
“Wengi wao wanamiliki magari, kwa hiyo huwa wanafanya ufuska humo. Kama una kinyaa, huwezi kuvumilia, ila ukiwa unapenda uchafu, basi panafaa,” alisema mtoa habari wetu mwingine.
Aunt, alipoulizwa kuhusu vitendo hivyo, alikiri Bongo Movie kugeuka danguro, akaongeza: “Ndiyo maana mimio nimejitoa.”
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ naye alikiri kuwepo tabia hiyo, akafafanua: “Mimi nashiriki asubuhi, tunafanya mazoezi ya mpira, wengine wanakutana usiku Leaders, hao ndiyo wanafanya ufuska, kwa hiyo mimi simo kwenye kundi hilo la usiku.”
JB: “Kuna kitu kinatubomoa Bongo Movie ndiyo maana mambo hayo yanasemwa, ukweli hii klabu imesaidia kupunguza uhasama wa wasanii kwa wasanii, maana wanakutana pamoja.” 
Jack Wolper: “Mimi nina zaidi ya miezi miwili sijakwenda Bongo Movie, nina kazi zinazonibana. Kwa upande wangu hata nikiwepo siwezi kuthubutu kutembea na mfanyakazi mwenzangu.”
Elizabeth Michael ‘Lulu ’: “Mtu kufanya mapenzi ni uamuzi wake, haina uhusiano na Bongo Movie.”
Sabrina Rupia ‘Catty’: “Umoja wa Bongo Movie unafurahisha, hilo suala la ngono na kuita danguro ni watu wachache wanaotaka kutuharibia.”
Single Mtambalike ‘Richie’: “Kwanza mimi nitakuwa mkali kama kweli hilo lipo. Naamini wanaosema hivyo ni wale wanafiki, wenye chuki na roho mbaya. Bongo Movie itadumu.”
Halima Yahya ‘Davina’: “Mimi sijui lolote, unajua mambo ya mapenzi ni siri, inawezekana wapo wanaopanga kufanya hivyo, lakini wanafanya siri, sisi wengine tutajuaje?”
Ruth Suka ‘Mainda’: “Kwa kweli kama kuna danguro sijui, ila Bongo Movie si danguro, kwani wasanii wakichukuana wenyewe kwa wenyewe ni danguro?”