Rais wa visiwa vya Maldives Mohamed Nasheed amejiuzulu baada ya wiki za maandamano yaliyoandamana na maasi ya maafisa wa usalama.
Akihutubia taifa kupitia runinga , Rais Nasheed alisema kwamba hali nchini humo itakuwa bora akiondoka.
Awali,polisi walioasi waliteka shirika la utangazaji la taifa jijini Male.
Taharuki ilkuwa imetanda baada ya jeshi la nchi hiyo kumkamata jaji mwandamizi mwezi uliopita; jambo lililozua maandamano makubwa katika visiwani hivyo vya Bara ya Hindi.
Sasa rais huyo anatarajiwa kuyakabithi madaraka kwa makamu wa rais Muhammad Waheed Hassan.
Awali Chanzo kiliambiwa kwamba kundi la maafisa wa polisi lilikuwa limeteka shirika la utangazaji la taifa, na kuanza kutangaza ujumbe wa kumuunga mkono rais wa zamani Maumoon Abdul Gayoom.