Mtanzania, Meja Jenerali Wynjones Kisamba, ambaye ni Kaimu Mkuu wa Majeshi ya Mseto wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur, Sudan, yajulikanayo kama UNAMID, akipokelewa leo asubuhi katika moja ya kambi za Majeshi hayo, nje kidogo ya mji wa El-Geneina, Darfur Magharibi, kuongoza zoezi la kuwavalisha medali za heshima za Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN) wanajeshi wa Nigeria wanaokaribia kumaliza muda wao wa kazi,
Wanigeria wakipita mbele yake kwa heshima tayari kurejea nyumbani. Aliwataka askari hao kuona fahari kuvishwa medali hizo na kwamba ziwe chachu katika kufanya kazi kwa nguvu mpya na kwa kuzingatia weledi na maadili ya hadi siku ya mwisho ya katika UNAMID. Kabla ya kujiunga na UNAMID mwaka jana akiwa Naibu Mkuu wa Majeshi yake, Jenerali Kisamba, ambaye amejizolea sifa tele kwa weledi wake hapa, alikuwa mkuu wa vikosi vya ardhini katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akipokea Saluti