Hili ni soko kubwa sana nchini Ubelgiji linaitwa Clemence,kila jumapili watu wengi hufanya shopping ya mahitaji yao ya vyakula kwenye soko hili.kwa kweli kuna kila aina ya vyakula na mchanganyiko wa madikodiko ya aina zote,leo nimepata bahati ya kutembelea soko hilo na jua lilikuwa kali sio mchezo.
Kama kawaida unapohemea inakubidi kufanya mambo ya kununua mazagazaga muhimu kwa ajili ya familia nyumbani.hapo tunapiga stori kidogo kuelekea kwenye dinga yetu turudi nyumbani.
Aisee mifuko ya plastiki ni nomaa kama unaibeba miingi halafu ikiwa mizito mmmh ni balaa utasema inakata vidole.hapo mzee mzima nakula pozi kidogo ili safari iendelee.
Tukapita kwa bwana Eddy ambaye ametupiga picha hii kupata madikodiko baada ya safari ndefu kutoka sokoni kuhemea madikodiko
Kazi na dawa,wakati wengine tunapiga msosi huku wengine wanaendelea kupata news kupitia Maganga One Blog ili kujua matokea ya mechi ya Simba na Waarabu.
0 Comments