Kumekuwa na shutma za kimataifa dhidi ya wanajeshi wa Mali waliopindua serikali ya rais Amadou Toumani Toure.
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka utawala wa kikatiba kurejeshwa nchini humo, huku Benki ya Dunia pamoja na Benki ya Maendeleo barani Afrika wakisema wanasitisha baadhi ya shughuli nchini humo.Msemaji wa wanajeshi waasi nchini Mali amesema jeshi litarejesha demokrasia nchini humo na kuwa umoja utarejea hivi karibuni.
Kufikia sasa haijulikani alipo Rais Amadou Toumani Toure, lakini taarifa ya televisheni ya taifa ilisema kuwa rais huyo yuko katika hali nzuri ya kiafya
0 Comments