Jirani kibaka akiwa kawekwa kwenye buti ya gari tayari kupelekwa kwa vyombo vya sheria.
Huyu jamaa alikua anatabia ya kuja dukani kwa sister na kuiba kwa mbinu za kijinga sana kisa dogo aliyekuwepo dukani alikua ni mgeni jijini, Siku ya kwanza alikuja na hela bandia akanunua soda kret zima moja halafu akatokomea nalo kusikojulikana. Mara ya pili akaja na gear nyingine alichofanya ni kumpatia dogo muuza duka hela kubwa, dogo alivyotoka kwenda kuomba chenji jama akazama kwenye droo ya hela akakomba elfu 50. Hili ni duka la vinywaji na ni la jumla. Jana tena kaja kwa gear ile ile lakini ikashindikana na akadakwa. Huyu jamaa ni mwenyeji wa tandika devis corner na ni kibaka mzoefu balaa. Nitaomba nikutumie na jina lake kamili siku za usoni ili kila mmoja amfahamu.hii ndio taarifa kamili kuhusiana na jirani yetu ambaye tunamuona kama jamaa yetu mzuri wa karibu! Kwani ni jamaa anayetufahamu sisi familia nzima,kiukweli inasikitisha sana. (Na Daniel wa Maganga One Blog)
0 Comments