Baada ya mgomo wa mabasi,Tram na Metro katika jiji la Brussel nchini Ubelgiji kwa takribani siku tano sasa,jana jioni hali ilibadilika na kuendelea vizuri baada ya kuona baadhi ya mabasi na tram zikifanya shughuli za usafiri kama kawaida.hali hii imesababishwa na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mabasi kuuwawa wiki iliyopita.
Wakati nipo ndani ya Tram nikapishana na tram nyingine ikiwa na abiria ndani,jambo ambalo halikuwepo kwa takribani siku tano sasa.tunamatumaini makubwa kwamba usafiri utaendelea vyema kwa masaa machache yajayo.
0 Comments