Kila mmoja alikuwa mtu mwenye uso wa furaha maana ilikuwa ni tabu kuamini kama kweli binaadamu mnaweza kupotezana kwa kipindi kirefu halafu mnakutana tena,ni miaka mingi sana tulipotezana na rafiki yangu Dulla mwenye shati lenye mistari ila tunashukuru Alhamdulillah tumekutana wazima.binafsi nimefurahi sana kukutana na swahiba wangu wa shule ya msingi.kulia kwa Dulla ni Manny.
Tukaanza kujikumbusha mambo ya shuleni jinsi tulivyokuwa tukigombea mihogo na chipsi za Tshs 20,yani ilikuwa furaha sana.kwa kweli siku ya leo ilikuwa burudani sana kwa upande wangu kwani ni muda mrefu sikuweza kuonana na huyu kijana wangu.
0 Comments