Mh. Balozi (katikati mwenye tai nyekundu) akisisitiza uhusiano wa kijamii
na utafiti mbalimbali baina ya mataifa hayo.

Mh.Balozi Hamza akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
waliotunukiwa zawadi, ama wambele walioketi kutoka kulia ni Profesa Saeed Atiah
Aly, Mkuu wa kituo cha lugha cha lugha ya kigeni na ukalimani. wapili ni Mh.
Balozi Mohamed Haji Hamza Balozi wa Tanzania Misri. watatu ni Professor Ali Ahmed Shaaban Mhadhiri Mkuu wa lugha za kigeni na
wa mwisho Nd. Idriss Kh. Juma Afisa
Mwandamizi katika Ubalozi wa Tanzania Cairo Misri.

Mh. Balozi Hamza akiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa idara na wahadhiri wa kituo
cha lugha za kigeni na tafsiri ya lugha za kiafrika katika chuo kikuu
cha Al-Azhar Cairo Misri.
  



 Mh.Balozi Mohamed Haji Hamza Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Misri, alikua ni mgeni rasmi katika sherehe maalum ya kuwatunuku wanafunzi waliofanya vizuri katika lugha ya kiswahili katika kitivu cha lugha za kigeni na tafsiri ya lugha za kiafrika katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar kilichopo mjini Cairo Misri.




Sherehe hiyo iliyofanyika tarehe 24 April 2012 kwenye ukumbi wa Chuo hicho.
Balozi Hamza amesifu ushirikiano wa siku nyingi uliokuwepo kati ya Misri na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya jamii.



Pia Mh. Balozi alisisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya chuo kikuu cha Al-Azhar na vyuo vikuu vya Tanzania katika kubadilishana wataalamu na watafiti pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka Tanzania kujiunga katika chuo hicho kila mwaka.