Mhasibu wa zamani wa duka la DIY mjini London ambaye alikuja kuwa gavana nchini Nigeria amefungwa jela miaka 13 kwa kufanya udanganyifu wa fedha karibu £50m ($77m).
James Ibori, gavana wa jimbo la Delta alikiri kujihusisha na makosa 10 ya ulaghai na biashara ya fedha haramu.
Mahakama ya Southwark Crown ilielezwa kuwa kiasi cha fedha alichoiba kutoka kwa watu wa jimbo la Delta kilikuwa ‘hakihesabiki’".
Ibori, aliyeepuka kukamatwa Nigeria baada ya kundi la mashabiki wake kuvamia kituo cha polisi, alikamatwa Dubai mwaka 2010.
Alihukumiwa Uingereza ambako alishtakiwa kwa ushahidi uliotolewa na Polisi wa London.
Mojawapo ya mashtaka yake Ibori alikiri kuhusika na udanganyifu wa kiasi cha $37m (£23m) kuhusu mauzo ya hisa za jimbo la Delta kwa kampuni ya simu nchini Nigeria iliyobinafsishwa ya V Mobile.
Alikuwa gavana wa Jimbo la Delta kati ya Mei 1999 na Mei 2007.
Wakili wa upande wa mashataka Sasha Wass, aliiambia mahakama kuwa Ibori "kwa makusudi na kwa mpangilio " aliwalaghai watu waliomchagua kuwawakilisha.

Mahakama pia iliarifiwa kuwa alikuja Uingereza miaka ya 1980 na kufanya kazi kama mhasibu wa duka la Wickes DIY huko Ruislip, kaskazini magharibi mwa London.

Kuinuka na kuanguka kwa James Ibori

1958: Alizaliwa Jimbo la Delta, Polisi wa Uinegereza wanaamini.
1980: Alihamia Uingereza
1991: Alishtakiwa kwa kuliibia duka la DIY, Wickes
1992: Alihukumiwa kwa udanganyifu
1993-4: Alijihusisha mwenyewe na utawala wa kijeshi waNigeriawa Sani Abacha
1999: Alichaguliwa gavana wa Jimbo la Delta
2007: Alijiuzulu kuwa gavana
2007: Uingereza ilitia tanjimaliyenye thamani ya $35m
Desemba 2007: Alikamatwa na mahakama ya Nigeria kwa tuhuma za rushwa.
2009: Mahakama ya Nigeria ilimfutia mashtaka
April 2010: Mashabiki wa Ibori walivamia kituo cha polisi wakijaribu kumkamata
Mei 2010: Alikamatwa Dubai
2011: Alihamishiwa Uingereza
2012: Alifungwa London
Alishtakiwa mwaka 1991 akiiba kwenye duka lakini alirejeshwa Nigeria na alianza kupanda kisiasa mpaka kwenye mtandao wa chama cha People's Democratic (PDP)
Alipowania ugavana alidanganya tarehe yake ya kuzaliwa kuficha uhalifu aliotuhumiwa kufanya Uingereza ambao ungemzuia kugombea nafasi hiyo.
Ibori, ambaye anwani yake ilitolewa kuwa ni Primrose Hill, Kaskazini mwa London, anadai kuwa na miaka 53 lakini polisi wa London wanasema ana miaka 49.
Alikuwa gavana mwaka 1999 lakini alianza kuchukua fedha za hazina za jimbo.

Alinunua:

  • Nyumba huko Hampstead,Londonkaskazini kwa £2.2m
  • Malikatika eneo la Shaftesbury,Dorset, kwa £311,000
  • Jumba la kifahari la kiasi cha £3.2m huko Sandton, karibu na Johannesburg, Afrika Kusini.
  • Gari ya kifahari lenye uwezo wa kuhimili mashambulio ya silaha aina ya zote [Range Rovers] yenye thamani ya £600,000
  • Gari aina ya Bentley £120,000
  • Gari aina ya Mercedes Maybach kwa Euro 407,000 ambayo ilisafirishwa kwenda katika jumba lake la kifahari Afrika Kusini
Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Sue Patten, mkuu wa kitengo cha mashtaka alisema mahakama itaomba mali zake zitaifishwe na kurejesha utajiri alioupata ‘kwa gharama ya baadhi ya watu maskini kabisa duniani’
Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Andrew Mitchell alisema: ‘Hukumu ya James Ibori inatoa ujumbe mzito na wa muhimu kwa wale wanaotaka kutumia Uingereza kuficha uhalifu wao wakiwa kama wakimbizi’
"Ufisadi ni saratani katika nchi zinazoendelea na serikali ya muungano haitavumilia hali hiyo."
Jumatatu kipindi cha BBC Newsnight kilionyesha kuwa mfuko wa misaada wa kitengo cha Uingereza cha maendeleo ya Kimataifa kinachoshughulikia miradi CDC Group, ukichunguzwa na maafisa wa Nigeria.
Kilifichua madai yanayoashiria kuwa CDC Group liliweka $47.5m (£29.9m) katika mfuko binafsi yaliyowekeza Nigeria yakituhumiwa kuhusishwa na Ibori.
DfID lilisema tuhuma hizo zilikuwa za mwaka 2009 na CDC, ambayo inayosimamiwa na Bw Mitchell, siku zote imekuwa ikifanya "uchunguzi wa makini " kabla ya kuwekeza kwenye mfuko huo.
CDC ilichunguza madai hayo wakati huo, na kukuta ‘hakuna dalili kuwa mfuko huo wa Uingereza umetumika vibaya", alisema.