Bodi ya Benki ya Dunia imemchagua mwanazuoni wa Marekani, Jim Yong Kim kuwa rais wa Benki hiyo.
Hii ni licha ya shinikizo kutaka nafasi hiyo kumuendea raia asiye mmarekani. Dkt. Kim ni mtaalamu wa Afya akiwa na uzoefu wa nchi zinazoendelea.Rais wa Benki ya dunia amekuwa daima akichaguliwa mgombea anaeteuliwa na Marekani. Awamu hii bodi ya Benki ya Dunia ilimteuwa Waziri wa fedha wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala.
Waziri huyo aliungwa mkono na nchi kadhaa zinazoendelea.Hata hivyo alikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wajumbe wanaopiga kura ambao wengi hutoka Ulaya na Marekani.
Rais wa sasa Robert Zoellick, anamaliza mhula wake wa miaka mitano hapo mwezi June.
0 Comments