Moja ya jitihada tunazozifanya wazazi nje ya nchi ni kuwafundisha watoto wetu maadili mema ya dini.tumeanzisha madrassa ili kuwaweka watoto wetu tofauti na watoto wa wenzetu ambao wamepewa uhuru zaidi katika mambo ya dunia.
Aliyesimama ni katibu wa Madrassa yetu mpya na aliyeketi akiwasikiliza wanafunzi wake ni mwalimu wetu mwenye kiwango kilichokubalika katika ufundishaji.
Kila mwanafunzi alikuwa bize kufanya kile alichoelekezwa na mwalimu wake,kwa kweli inatupa moyo na kutufurahisha wazazi juu ya hili tulilolianzisha.Mungu awape moyo wa kujiendeleza kielimu watoto wetu.
Watoto wetu wakimaliza kusoma,hufundishwa taratibu zote za kufanya Ibada na pindi wakimaliza kufanya Ibada kama kuna vinywaji au vitafunwa basi wanajiburudisha kwa njia hiyo kama unavyowaona pichani.
Kwa kuwa hata mchicha ulianza kama mbuyu basi na sisi tumeanzisha madrassa kwa ufinyu wa watoto insh`Allah watakavyozidi kuzoea watakuja na wengine.