Msanii wa kizazi kipya cha Bongo Flava Chege Chigunda mtoto wa mama Said mwenye maua mkononi akipata picha ya pamoja na watu wake wa karibu kabisa waliofika Airport kumlaki alipowasiri jioni ya jana nchini Holland.
King James kushoto akiwa na mshirika wake Dj G Town walipofika airport na fans wa Chege chigunda kumpokea kwa ajili ya show ya mkesha wa pasaka siku ya jumapili hapo jijini Amsterdam
Kila mmoja alipenda kumpa sapoti kijana wetu wa nyumbani Chege Chigunda alipowasiri Amsterdam Airport tayari kwa ajili ya show siku ya mkesha wa pasaka.
Kila mmoja meno nje kwa furaha na upendo,ni Chege Chigunda mtoto wa Tmk alipowasili kwa akijli ya show kwenye mkesha wa pasaka tarehe 8 April 2012.
Inapendeza sana kuona watanzania,waganda,waburundi,wakenya,wanyarwanda,waethiopia wanashiriki vyema katika kupeana sapoti nje ya nchi.kwanza tunakuza majina ya wasanii wetu,pili tunadumisha Ushirikiano wetu na tatu ule upendo wetu wa asilia ambao tumerithishwa ndio unatufanya kuwa kitu kimoja,nawapongeza sana waandaji wa hii show kwa kuwa na umoja.
 Fyatua babu fyatuaaa  fyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.........!!!!!
Hapo ni kuuza mpaka kukopesha kabisa
Ni moja ya kumbukumbu nzuri kwa wasanii wetu na mapromota zetu wanaojitahidi kwa hali na mali kuwatangaza wasanii wetu nje za nchi,hii inaleta changamoto kwa wenzetu walioendelea kuwa nasi tumeamka na kuheshimu kazi zetu.viva east Afrika kwa ujumla.
Hapo jeeee? waungwana mabibi na mabwana show hii sio ya kukosa kwani Chege amejipanga vya kutosha ili kuwaburudisha watu wake siku ya mkesha wa pasaka,ukikosa show hii ni sawa na umejidhulumu nafsi yako.