Mkuu wa Polisi nchini, Inspekta wa Polisi, Saidi Mwema |
Mkuu wa Polisi nchini, Inspekta wa Polisi, Saidi Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa mahafali ya wahitimu zaidi ya 3,210 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi.
Alisema hakuna anayependa nchi kuingia katika machafuko na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na amani na utulivu bila kusababisha nchi kuingia katika machafuko.
“Kwa sasa sehemu mbalimbali kuna chaguzi ndogo ndogo za kata na
majimbo, tunawataka wananchi wanapomaliza kupiga kura kuondoka kwenye kituo cha kura na kurejea nyumbani kusubiri matokeo na si kukaa kwenye vituo vya kupigia kura,” alisema Mwema
Aliongeza kuwa, jukumu la Jeshi la Polisi ni kuhakikisha usalama
wa wananchi na mali zao unakuwepo na hawataacha kutekeleza kazi zao ili kuhakikisha nchi inakuwa katika hali ya amani muda wote.
Aidha, aliwaomba wananchi wa maeneo hayo, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa polisi ili kufanya zoezi la ulinzi na usalama kwa raia kukamilika bila bugudha.
Jimbo la Arumeru leo wananchi wanatarajia kupiga kura kumchagua mbunge wa kuwawakilisha kwa kipindi cha miaka mitatu iliyobaki kabla ya kufikia uchaguzi mkuu mwaka 2015, baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Sumari.
0 Comments